Mubarak alichuka kusikia Qur'ani ikisomwa

  • Habari NO : 263637
  • Rejea : IRNA
Brigidia Jenerali Shafiq al-Banna ambaye alikuwa mkuu wa gadi ya ulinzi wa Ikulu ya Misri katika kipindi cha utawala wa dikteta Hosni Mubarak wa nchi hiyo amesema kuwa dikteta huyo daima alikuwa mlevi ambaye alichukia sana kusikia Qur'ani Tukufu ikisomwa mbele yake.

Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bait(a.s)-ABNA-Brigidia Jenerali Shafiq al-Banna ambaye alikuwa mkuu wa gadi ya ulinzi wa Ikulu ya Misri katika kipindi cha utawala wa dikteta Hosni Mubarak wa nchi hiyo amesema kuwa dikteta huyo daima alikuwa mlevi ambaye alichukia sana kusikia Qur'ani Tukufu ikisomwa mbele yake.

Amesema katika kipindi kimoja cha televisheni kwamba dikteta huyo alikuwa akiwahadaa watu kwa kudhihiri kwenye kikao cha mwisho cha kila mwaka cha kufunga mashindano ya Qur'ani Tukufu ili kuonyesha kuwa ndiye aliyekuwa akisimamia mashindano hayo, katika hali ambayo mwenyewe alikuwa akichukia sana kusikia aya za Qur'ani zikisomwa. Amesema mbali na sherehe muhimu za Kiislamu kama vile Idul Fitr na minasaba mingine muhimu ya kidini, hakuwahi kumwona Mubarak akiswali na kwamba hata hakuwa akihudhuria swala za Ijumaa zilizoswaliwa katika misikiti tofauti ya Misri.

Shafiq al-Banna ambaye tokea mwaka 1975 hadi 2000 alikuwa akiandamana na Mubarak kila sehemu aliyoenda, amesema kuwa dikteta huyo daima alikuwa mlevi ambaye hakutaka kusikia Qur'ani ikisomwa na kwamba mwanawe Alaa tu ndiye aliyekuwa akiswali katika familia ya dikteta huyo. Amesema Jamal Mubarak kama alivyokuwa baba yake, hakuwa akiswali isipokuwa kwenye minasaba maalumu ya kidini tena akiwa na walinzi wengi ili kuwavutia watu.

Brigidia Jenerali Shafiq al-Banna amesema kuwa Mubarak alipiga marufuku kuzungumzwa mambo kama vile mauti, swala, Qur'ani na masuala mengine mbele yake kwa sababu yalimchukiza sana. Ameongeza kuwa anaamini Jamal Mubarak ndiye aliyekuwa chanzo hasa cha kuanguka utawala wa dikteta huyo wa zamani wa Misri.


Mourining of Imam Hossein
بی کفایتی آل سعود
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky