Vikao vya kiraa ya Qur'ani kufanyika Iraq sikukuu ya Ghadir

  • Habari NO : 277910
  • Rejea : tehran
Vikao vya kuanisika na kiraa ya Qur'ani Tukufu vimepangwa kufanyika katika mikoa mbalimbnali ya Iraq katika sikukuu ya Ghadir Khum inayosadifiana na Jumanne ya wiki ijayo.
Vikao vya kuanisika na kiraa ya Qur'ani Tukufu vimepangwa kufanyika katika mikoa mbalimbnali ya Iraq katika sikukuu ya Ghadir Khum inayosadifiana na Jumanne ya wiki ijayo.
Raad Adnan ambaye ni Mratibu wa Kamati Kuu ya Qur'ani Tukufu ya Iraq katika mkoa wa Dhiqar amesema vikao na makongamano hayo ya Qur'ani yatafanyika katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya Ghadir katika mikoa mbalimbali ya Iraq.
Amesema kuwa vikao hivyo vya kiraa ya Qur'ani vinafanyika kwa kutilia maanani hadithi ya Bwana Mtume (saw) ambaye amesema: "Ali yuko pamoja na Qur'ani, na Qur'ani iko pamoja na Ali, na viwili hivyo havitatengana hadi vitakaponikuta mimi katika hodhi ya Kauthar."
Siku ya terehe 18 Dhulhija ni sikukuu ya Ghadir ambamo Waislamu wafuasi wa Ahlul Bait hukumbuka tukio la kutawazwa rasmi Ali bin Abi Twalib (as) kuwa Imam na kiongozi wa Waislamu wote baada ya Mtume (saw)
بی کفایتی آل سعود
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky