1 afariki na 6 kujeruhiwa katika maandamano ya Basrah nchini Iraq

1 afariki na 6 kujeruhiwa katika maandamano ya Basrah nchini Iraq

Maandamano yaliofanyika usiku wa jana katika mji wa Basrah nchini Iraq yamepelekea kupoteza maisha mmoja katika waandamanaji hao na wengine sita kujeruhiwa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyanzo vya habari nchini Iraq leo vimetangaza kuuwawa kwa mtu mmoja miongoni mwa waandamanaji na wengine sita kujeruhiwa katika vuruhugu ziliotokea usiku wa jana kati ya waandamanaji na majeshi ya ulinzi na usalama nchini humo.
Waandamanaji hao walionekana wakuwarushia mawe majeshi ya ulinzi na Usalama wa nchi hiyo, ambapo majeshi ya usalama nayo yalilazimika kutumia mabomu ya machozi na kurusha risasi hewani.
Idadi ya waandamanaji walioshiriki katika maandamano hayo ni watu 700 au 600 ambao waliandamana kwaajili ya kufikisha ujumbe wao unaoashiria hali ngumu ya maisha nchini humo na uchache wa huduma za serikali kwa wananchi.
Aidha Inasemekana kwamba waandamanaji nchini humo wametoa malalamiko kuhusu dhulma inayofanywa na viongozi wa serikali hiyo na kupungua kwa huduma za serikali kwa wananchi ikiwemo kukatika kwa umeme kwa muda mrefu, ukatikaji wa maji nk.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky