Al-abadi: baada ya kuwaondosha magaidi wa Daesh, tupo katika kuijenga upya Ira

Al-abadi: baada ya kuwaondosha magaidi wa Daesh, tupo katika kuijenga upya Ira

Haidary Al-abadi amesema: Iraq imeanza hatua nyingine ya kujenga na kufanya juhudi za kuirudisha hali ya uchumi katika kawaida yake katika maeneo yote nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri mkuu wa Iraq, ameyasema hato  leo katika maazimisho ya miaka 96 ya kuasisiwa jeshi la Polisi la nchi hiyo na kusema kuwa: majeshi ya ulinzi na usalama ya Iraq kwa ushirikiano wa sekta zao zote bado zinaendelea kuwasaka magadi wa Daesh waliokuwa wamesambaratishwa, ambapo baadhi yao wamekimbilia katika majangwa na sehemu mbali mbali za maficho.
Aidha Al-abadi ameongeza kusema kuwa: Iraq hivi sasa inafanya juhudi kubwa ya ujenzi wa maeneo yalioharibiwa na kurudusha hali ya uchumi katika hali yake ya kawaida katika maeneo yote ya taifa, hatimaye kuushinda uchumi kama tulivyooshinda ugaidi na kuwapatia maisha bora wananchi wa wetu.
Mwisho amemalizia kwa kuashiria nafasi na umuhimu wa majeshi ya ulinzi na usalama na wizara ya mambo ya ndani ya Iraq kwa kushikamana kwao katika kukabiliana na ugaidi hata kuusambaratisha kwake.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky