Ansarullah: tuko tayari kubadilishana mateka na Saudi Arabia

 Ansarullah: tuko tayari kubadilishana mateka na Saudi Arabia

Mkuu wa kikundi cha wanamapinduzi wa Yemen amesema: tuko tayari kubadilishana mateka na Saudi Arabia sawasawa kupitia chama msalaba mwekundu au mubashara na Saudi Arabia, kama tulivyokuwa tumetangaza hapo awali

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi mkuu wa kamati kuu ya wanamapinduzi wa Yemen ametangaza utayari wao wa kubadilishana mateka na Saudi Arabia.
Hayo yamesemwa na (Sayyed Muhammad Ali Alhuthiy) ambaye ni mkuu wa kamati kuu ya wanamapinduzi wa Yemen kunako kubadilisha mateka wa Saudi Arabia waliokuwa mikononi mwao na wale wa Yemen waliokuwa mikononi mwa Saudi Arabia.
Hayo aliandika katika ukurasa wake wa Twitter: tuko tayari kubadilishana mateka na Saudi Arabia, kwa njia yeyote hile sawasawa kupitia chama cha msalaba mwekundu au mubashara na Saudi Arabia, kama tulivyokuwa tumeashiria suala hilo hapo awali katika vikao vyetu, pia jambo hilo tumelisisitiza tulipokuwa pamoja na chama cha Msalaba mwekundu.
Huku kwa upande mwingine majeshi ya Yemen yakiendeleza mashambulizi yake dhidi ya majeshi ya kivamizi nchini humo ambapo yameonekana kusonga mbele katika jangwa la (Al-baqa) katika mji wa Swadah na Najrani ambapo imepelekea kufa majeshi ya Rais wa Yemen aliejiengua na majeshi ya umoja wa Waarabu na wengine wengi kujeruhiwa katika sehemu hiyo.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
We are All Zakzaky