Balozi wa Emirates auwawa nchini Afghanistan

Balozi wa Emirates auwawa nchini Afghanistan

Balozi wa Emirates nchini Afghanistan ameuwawa kutokana na majaraha makubwa alioyapata kufuatia mripuko wa kigaidi uliokuwa umetokea katika mji wa Qandahar nchini humo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: balozi huyo nchini Afghanistan amekufa baada ya kupata majaraha makubwa katika mripuko uliotokea hivi karibuni katika mji wa Qandahar.
Serikali ya Emirates baada ya kutangaza habari hiyo imesema: “Juma Al-Kabiy” ambaye ni balozi wa Emirates nchini Afghanistan amekufa baada ya kuwa na majaraha makubwa alioyapata katika mripuko wa kigaidi uliotokea hivi mweshoni nchini Afghanistan.
Mripuko uliosababisha kifo cha balozi huyo nchini Afghani ulitokea katikati ya mwezi Januari mwaka huu katika hoteli moja iliopo mjini Qandahar na kupelekea kujeruhiwa watu wanane ikiwemo balozi huyo.
Mripuko huo ulitokea muda ambao mkuu wa mkoa wa Qandahar alimkaribisha balozi huyo katika hoteli hiyo, ambapo pia katika mwaliko huo mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Qandahar na mkuu wa masuala ya usalama walikuwa pamoja sehemu hiyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky