Ghala la silaha la majeshi ya Saudi Arabia laripuka kufuatia shambulio la majeshi ya Yemen

Ghala la silaha la majeshi ya Saudi Arabia laripuka kufuatia shambulio la majeshi ya Yemen

Vyanzo vya habari vya Yemen vyatangaza kufanya shambulio kwa makombora ya majeshi hayo katika ghala la silaha la Saudi Arabia liliopo katika kusini mwa Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yametangazwa na kikosi cha makombora katika majeshi ya Yemen kwamba, ghala la silaha na vifaa vingine vya kijeshi vya Saudi Arabia limeripuka kufuatia makombora yaliorushwa na majeshi ya Yemen sehemu ya Jizani kusini mwa Saudi Arabia.
Aidha vyanzo vya habari vya Yemen vinasema kuwa: ghala la silaha na vifaa vingine vilipuka kwa mripo mkubwa kutokana na shambulio ambapolimefanywa na majeshi ya Yemen.
Kadhalika chanzo kimoja cha majeshi ya Yemen kimesema kuwa ghala hilo limeripuliwa na Kombora aina ya Zilzala1 katika sehemu hiyo, kwa upande mwinge pia kumeripotiwa kuangamizwa kwa gari moja kubwa la Saudi Arabia katika mji wa Al-hudaidah nchini humo.
Aidha gari liliokuwa limesambaratishwa na majeshi ya Yemen lilikuwa limebeba silaha na vifaa vya vita vya Saudi Arabia nchini Yemen.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky