Iraq yaingia hasara ya Dola bilioni 100 katika vita ya kupambana na magaidi wa Daesh

Iraq yaingia hasara ya Dola bilioni 100 katika vita ya kupambana na magaidi wa Daesh

Waziri mkuu wa Iraq leo ametangaza kuwa katika vita ya kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh Iraq imeingia hasara takriban ya dola bilioni 100 za Kimarekani nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri mkuu wa Iraq leo ametangaza kuwa nchi yake imepata hasara ya kiasi cha Dola bilioni 100 katika vita ya kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
“Haider Al-abadi” amebainisha kuwa: mushkili mkubwa wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ni fikra zao, hivyo tunapaswa kupambana na kikundi hicho na kujipanga ipasavyo katika kukabiliana nacho kwani fikra yao ni kusambaratisha wananchi wasiokuwa na hatia.
Aidha ameendelea kusema kuwa; munapaswa kujiepusha na kueneza masuala ya kuleta vitina kwa kutumia mitandao ya kijamii, kwa lengo la kuwatisha wananchi, kwani kuna watu maalumu wanaotoa mali zao kwaajili ya kueneza fitina katina baina ya wananchi wa Iraq jambo ambalo hawataweza kulifikia.
Waziri mkuu wa Iraq mwisho amebainisha kuwa: nimeshatoa maagizo kwa jeshi la ulinzi na usalama wa taifa kwamba wale wote ambao hufanya juhudi za kuleta fitina katika jamii, wakamatwe hara iwezekanavyo na kufikishwa mahakamani.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky