Japan Yazindua Misikiti Unaotembea kutumika Olimpiki Tokyo

Japan Yazindua Misikiti Unaotembea kutumika Olimpiki Tokyo

Japan imezindua 'misikiti inayotembea' ambayo itatumika katika Michezo ya Olimpiki na Paralimpiki Tokyo mwaka 2020.

Waandalizi wa michezo ya olimpiki Tokyo wanasema 'misikiti' hiyo ambayo kimsingi ni vyumba vya kusalia itakuwa katika makao ya wanariadha katika michezo hiyo.

Misikiti hiyo inayotembelea itaweza kukidhi mahitaji ya Waislamu watakaofika katika mji huo wenye misikiti michache.

Shirika linalohusika na mradi huo lilizindua sampuli ya msikiti huo hivi karibu katika mji wa Toyota jimboni Aichi. Shirika hilo limekarabati trela ambayo ina chumba kinachoweza kutumiwa na waumini 50 wakati moja na pia kuna kuna dira inayoonyesha qibla. Aidha msikiti huo una vifaa vyote vya kujinadhifisha na kuchukua udhu kabla ya kuswali.

Trela hiyo inagharimu takribani dola za Kimarekani 900,000 lakini shirika husika linalenga kupunguza bei hiyo.

Ubunifu huo ni wa Yasuharu Inoue, mkaazi wa Tokyo ambaye ni mwenyekiti wa shirika moja ambalo huhusika na uandaaji hafla. Inoue alitoa huduma mbali mbali mbali katika michezo ya Olimpiki ya Athens mwaka 2004 na London mwaka 2012 na hivyo analenga kutumia Michezo ya Olimpiki ya Tokyo kuwa fursa ya kuwaleta pamoja wanariadha na washiriki wa kigeni na Japan.

Akifafanua kuhusu mradi wake Inoue anasema: "Sala ni katika nguzo muhimu za Waislamu. Nataka kuwakaribisha Waislamu (katika michezo ya Tokyo ya 2020) kwa ukarimu wa Kijapani kwa kuwapa mazingira tulivu ya kufanya ibada."

Inoue anasema ameshirikiana na mashirika kadhaa ya Japan ya kutegeneza magari ili kuchora ramani bora ya 'Misikiti Unaotembea'.

Anasema  wanalenga kutegeneza misikiti 10 ifikapo 2020 ili wanariadha Waislamu na washiriki wengine Waislamu katika Olimpiki waweze kutumia maeneo hayo ya ibada.
...............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky