Jeshi la Polisi la Iraq lakamata magaidi wa Daesh 12 mjini Kirkuk

Jeshi la Polisi la Iraq lakamata magaidi wa Daesh 12 mjini Kirkuk

Majeshi ya ulinzi na usalama nchini Iraq yametangaza kukamatwa kwa magaidi 12 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Kirkuk nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya ulinzi na usalama nchini Iraq yametangaza kukamatwa kwa magaidi 12 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Kirkuk nchini humo.
Aidha majeshi hayo ya ulinzi yamefanikisha suala hilo kwaushirikiano wa majeshi ya kukabiliana na ugaidi nchini humo na kuashiria kufanikiwa kukamata magaidi 12 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Kirkuk ambapo walikuwa wamejificha katika mji huo.
Inasemekana kwamba mpango wa kuwasaka magaidi waliobaki nchini humo bado unaendelea katika maeneo ya magharibi ya kusini mwa Kirkuk na mashariki mwa mkoa wa Saladin na maeneo mengine ya Iraq.
 mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky