Jeshi la Urusi lagundua ghala la silaha za magaidi nchini Syria

Jeshi la Urusi lagundua ghala la silaha za magaidi nchini Syria

Moja kati ya magahala makubwa ya silaha zinazomilikiwa na vikundi vya kigaidi lagunduliwa kaskazini mwa mkoa wa Hums nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Urusi nchini Syria yametangaza kugundua ghala lubwa la silaha ambazo ni miliki ya vikundi vya kigaidi kaskazini mwa mkoa wa Hums nchini humo.
Aidha majeshi ya Urusi yamezipata picha na kanda za video ziliokuwa zimeandaliwa na magaidi hao na kuzirusha katika mitandao mbalimbali.
Majeshi ya Urusi nchini Syria yalikuwa yakifanya dolia katika maeneo ya Rastan, ndipo wakagundua kuwepo kwa ghala hilo liliokuwa na idadi kubwa ya vifaa vya vita ikiwemo makombora na kemikali za miripoko.
Inasemekana kwamba ghala la sihala hizo ni lamagaidi ambao walikuwa wameiteka sehemu hiyo, ambapo kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano walihama sehemu hiyo na kwenda sehemu nyingine.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky