Jeshi la Yemen lafanya shambulio katika mji mkuu wa Saudia kabla ya masaa kadha ya kufika Rais wa Marekani

Jeshi la Yemen lafanya shambulio katika mji mkuu wa Saudia kabla ya masaa kadha ya kufika Rais wa Marekani

Majeshi ya Yemen usikuwa wa Jumamosi yamefanya shambulio la kombora la masafa marefu katika mji mkuu wa Saudi Arabia, katika hali ambayo serikali ya Saudi Arabia ilikuwa katika maandalizi ya kuupokea msafara wa rais wa serikali ya Marekani nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Yemen yameshambulia mji mkuu wa Saudi Arabia kwa kombora la masafa marefu aina ya Berkane namba 2 nchini humo.
Televishen ya Almasirah imetangaza katika habari yake ikinukuu kutoka kwa msemaji wa majeshi ya Yemen kwamba: ujumbe wetu tuliotuma kwa Kombora hilo, ni ishara ya kwamba sisi tuko imara kukabiliana na aina yeyote ya uvamizi wa mataifa ya kidhalimu.
Hayo yamesemwa na Sharafu Lukuman “msemaji wa majeshi ya Yemen” kuwa ujumbe wetu umewafikia wasaudia ni tunawaambia kuwa tuko tayari kujibu mashambulizi na kukabiliana na maadui wa Yemen.
Shambulio hili limefanyika usiku wa kuamkia Jumamosi, ambayo serikali ya Saudia ilikuwa katika kuandaa mazingira ya kuupokea msafara wa Rais wa Marekani nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hii ni kwamba shambulio hilo lilifanywa kabla ya masaa kadhaa ya kuwasili kwa rais wa Marekani “Donald Trump” katika mji mkuu wa nchi hiyo (Riyadh), ambapo kufuatia shambulio hilo, uwanja wa ndege wa Malik Halidi ulisitisha kurusha ndege kutoka katika uwanja huo kwa muda kadhaa.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky