Kamanada wa kikoso maalumu cha wanawake wa Daesh aenguliwa

Kamanada wa kikoso maalumu cha wanawake wa Daesh aenguliwa

Umu Yasir Almuhajir ambaye ni kamanda na kiongozi wa kikosi cha wanawake katika kikundi cha kigaidi cha Daesh “maarufu kama Alhusana” aenguliwa katika nafasi hiyo kwa kosa la kuto tekeleza amri ya mkuu wa kikundi hicho cha kigaidi nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda na kiongozi wa kikosi cha wanawake wa kikundi cha kigaidi cha Daesh maarufu kama (Alhusana) wamemvua cheo hicho baada ya kukiuka maagizo ya viongozi wa kikundi hicho.

Kikundi cha kigaidi cha Daesh kimemuengua kamanda na kiongozi wa kikosi cha wanawake (Umu Yasir Almuhajir) katika nafasi hiyo kwa kosa la kukiuka amri za kiongozi mkuu wa kikundi hicho, amri ambayo ilikuwa inamtaka kuwachapa viboko wanawake katika soko la Tal Afar, hivyo alienguliwa katika nafasi hiyo na kukusimikwa binti mmoja katili zaidi kutoka nchini Ujerumani.

Binti huyo alioanishwa kuwa kiongozi wa kikosi hicho alikuwa kiongozi muhimu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mkoa wa Neneveh nchini Iraq.

Inasemekana kwamba kikosi maalumu cha magaidi wakike wa Daesh “Alhasana” ni katika vikundi vinavyofungamana na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambacho kazi yake kusimamia kanuni ngumu za kikundi hicho katika miji mbalimbali inayokaliwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ikiwepo pia kufanya dolia katika barabara za miji hiyo.

Miongoni mwa nyadhifa za kikundi hicho ni kuzuia fungamano lolote baina ya wanawake na wanaumi na kukabiliana na vitendo vya kimagharibi katika barabara za mji wa Musol kabla haijakombolewa.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky