Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa ampongeza Rouhani kwa ushindi wa Urais

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa ampongeza Rouhani kwa ushindi wa Urais

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ametoa pongezi za dhati kwa wananchi wa Iran kwa kukamilisha zoezi la uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo huku akimpongeza Rais Rouhani kwa ushindi mkubwa aliopata katika uchaguzi huo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa huku akisisitiza kuwa, kukamilika kwa zoezi la uchaguzi wa Urais na kumpata Rais mpya wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran ni jambo lakufurahisha na lenye kutia matumaini
Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa ametangaza baada ya kutoa pongezi zake kwa Rais mteule amesema: katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anashauku kubwa ya kuendeleza ushirkiano na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta mbalimbali.
Viongozi mbalimbali wa matifa mbalimbali wamempongeza Rais Rouhani kwa ushindi mpya aliopata katika uchaguzi mkuu wa kumtafuta Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika tarehe 19 mwezi huu, ambapo Hasan Rouhani ndiye alieibuka na ushindi wa kishindo katika nafasi hiyo, hivyo kufanikiwa kuchukua nafasi hiyo tena kwa mara ya pili.
Aidha katika uchaguzi uliofanyika siku ya Ijumaa iliopita ya tarehe 19 Hasan Rouhani alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa kupata asilimia 57 za kura ziliopigwa na wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura nchini Iran na kura hizo ndizo ziliomfanya Rouhani kuwa Rais wa awamu ya 12 katika nchi hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky