Katibu mkuu wa umoja wa mataifa asisitiza kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyuklia

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa asisitiza kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyuklia

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesisitiza kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Irana kwa maana makubaliano hayo ni moja kati ya makubalino makubwa kwaajili ya amani ya dunia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na mkuu wa umoja wa mataifa “Antonio Guterres” alipokuwa akizungumzia kuthibiti kwa usalama wa ukanda wa mashariki na kati, na akionyesha khofu na hali ya amani ya ukanda huo endapo yatatelekezwa makubaliano hayo.
Aidha amesema katika kikao kilichofanyika katika Balaza la usalama la umoja wa mataifa kuwa: makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran, ni moja kati ya makubaliano makubwa muhimu ya kuhifadhi suluhu na usalama duniani.
Kwa mujibu wa ripoti ziliopo ni kwamba Rais wa Marekani alitangaza kutoka katika makubaliano hayao mwezi mmoja uliopita na kuahidi kuvirudisha vikwazo vyote dhidi ya Iran.
Pamoja na hali hiyo Urusi, China na wengine waliokuwa wameshiriki katika makubaliano hayo wamepinga vibaya maamuzi ya kutoka kwa Marekani katika makubaliano hayo, huku wakisisitiza kuwa wataendelea kubaki katika makubaliano hayo baada ya kutoka kwa  Marekani.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky