Kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi Daesh amepatwa na saratani ya Figo

Kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi Daesh amepatwa na saratani ya Figo

Tovuti mmoja ya Iraq imedai kuwa kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh amepatwa na ugonjwa wa Saratani ya Figo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: chanzo kimoja chenye mamlaka ya juu, ametangaza kuwa Abubakari Al-baghdadi ambaye ndiye kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, amepatwa na ugonjwa wa Saratani ya Figo na hivi sasa anasumbuliwa vibaya sana na ugonjwa huo.
Tovuti ya leo Baghdai ikinukuu kutoka kwa chanzo makini nchini humo na kuandika kuwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh amepatwa na ugonjwa mbaya wa Saratani ya Figo ambapo kwa sasa yupo na hali mbaya akisumbuliwa na ugonjwa huo.
Chanzo hicho kimesema kuwa inawezekana hivi karibuni kikundi hicho kinaweza kuchagua kiongozi mwingine na kumtangaza.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky