Kupambana na majeshi ya ulinzi ni mstari mwekundu

Kupambana na majeshi ya ulinzi ni mstari mwekundu

Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Iraq na kusisitiza kuwa kushambulia majeshi ya usalama ya nchi hiyo inahisabiwa ni mstari mwenkundu

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Haider Al-abadi “waziri mkuu wa Iraq ameyasema hayo alipokuwa katika kongamano la kila wiki mjini Baghdadi na kusisitiza kuwa: serikali inafanya na kufuatilia watu ambao walighushi katika uchaguzi uliopita ambapo mahakama ya nchi hiyo pia imetoa mashtaka dhidi ya watu hao.
Aidha ameongeza kusema kuwa: kwaajili ya kukabiliana na ufisadi nchini, tunahitaji nguvu kubwa zaidi ya kufanya uchunguzi ambapo utatufanya kukabiliana na vikundi vya kigaidi, ambapo pia upande wa  mahaka tunaitaka iongeze juhudi katika kuwathibiti mafisadi pia kuzuia kukithiri kwa ufisadi nchini humo.
Al-abadi amefafanua kuwa: mashambulizi ya kulipiza mauaji ya mashahidi imetusababishia kufukia tija nzuri ya kuwatia mbaroni magaidi waliobaki, jambo ambalo limepelekea magaidi kuto pendwa na wanchi nchini humo.
Aidha kuhusu hali ya mabadiriko ya Syria alibainisha kuwa, kutokea marumbano kati ya mataifa hayo mawili ni katika mambo ambayo yatapelekea kurejea kwa magaidi wa Daesh katika mipaka ya Iraq na kurejea hatari ya kikundi hicho nchini humo.
Waziri mkuu wa Iraq ameashiria marumbano yaliotokea kati ya waandamanji na majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo katika baadhi ya miji ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa: kushambulia majeshi ya usalama linahesabiwa kuwa ni mstari mwekundu, ambapo hatutalinyamzia suala hilo.    
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky