Magaidi 10 hatarI wakamatwa katika mji wa Musol nchini Iraq

Magaidi 10 hatarI wakamatwa katika mji wa Musol nchini Iraq

Wizara ya mambo ya ndani ya Iraq imetangaza kuwa: magaidi kumi hatari wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wamekamatwa katika mji wa Musol

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Iraq ametoa tamko kuwa kamanda wa kanda maalumu ya Nineveh amefanikiwa kuwatia mbaroni magaidi 10 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika dolia nzito walioifanya katika kanda hiyo.
Aidha ameongeza kusema kuwa: miongoni mwa magaidi kumi hao ni miongoni mwa viongozi wa kikundi hicho ambao walikuwa wazimamizi wa mauaji ya watu na kupanga mbinu za kufanya miripoko katika miji mbalimbali katika sehemu hiyo.
Waziri mkuu wa Iraq ambaye ndio amirijeshi mkuu wa majeshi ya Iraq, mnamo tarehe 31 mwezi wa nane mwaka 2017, alitangaza kukombolewa kikamilifu mkoa wa Nineveh kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaiodi cha Daesh.
Majeshi ya Iraq mwezi wa nane 2017 aliwafanikiwa kuukomboa mkoa wa Nineveh mji wa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh ambao waliofanya mji huo kuwa ni makao makuu ya magaidi hao.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky