Magaidi 14 wa kikundi cha Daesh wakamatwa nchini Uturuki

Magaidi 14 wa kikundi cha Daesh wakamatwa nchini Uturuki

Magaidi 14 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wakamatwa nchini Uturuki kupitia Dolia za jeshi la kukabiliana na miripuko nchini Uturukivya

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jeshi la Polisi la kupambana na miripuko katika mji wa Adana nchini Uturuki wamefanikiwa kuwakamata magaidi 14 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika dolia walioifanya wakishirikiana na jeshi la nchi hiyo.
Aidha walipokuwa wakifanya uchunguzi katika makazi ya watuhumiwa hao, wamegunduwa kumiliki vifaa mbalimbali kisasa vinavyo husiana na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Taifa la Uturuki ni katika mataifa muhimu iliotumika kupita magadi wa vikundi mbalimbali kwenda nchini Syria wakitumia sehemu ya kusini mwa Uturuki, ambapo magaidi hao baada ya kuingia Syria walifanikiwa kuingia nchini Iraq na kufanya mauaji mazito ya kinyama katika mataifa hayo.
Hivi karibu waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki ametangaza kuwepo kwa magaidi wa Daesh waliofungwa katika nchi hiyo kuwa ni magaidi elfu kumi.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky