Magaidi 6 wa Daesh waangamia kaskazini mwa Iraq

Magaidi 6 wa Daesh waangamia kaskazini mwa Iraq

Magaidi 6 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh waangamia wakiwemo makamanda wa kikundi hicho kaskazini mwa Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Muin As-sadiy amabye ni kamanda wa majeshi ya Iraq yaliopo katika mkoa wa Kirkuk ambapo amesisitiza kwa kusema kuwa: magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ambao walikuwepo katika vilele vya milima ya Hamrin katika mkoa wa Kirkuk, yameshambuliwa na majeshi ya anga ya Iraq katika sehemu ya milima hiyo, ambapo kufuatia mashambulio hayo magaidi 6 wa kikundi hicho wamepoteza maisha ikiwemo viongozi wao.
Aidha aliongeza kusema kuwa: mashambulio hayo yamepelekea kumuangamiza kamanda mmoja wa masuala ya kijeshi katika kikundi hicho ambaye aliokuwepo katika sehemu ya Dabsi, alkadhalika kamanda mwingine wa masuala ya kutengeza miripuko katika sehemu mbalimbali, naye ameangamia kufuatia mashambolio hayo.
 Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa: hali ya usalama katika mkoa wa Kirkuk iko vizuri, ambapo maandalizi ya kusherehekea sikukuu ya Newruzi yameanza.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky