Magaidi elfu moja waweka silaha chini sehemu ya Homeh ya Deraa nchini Syria

Magaidi elfu moja waweka silaha chini sehemu ya Homeh ya Deraa nchini Syria

Magaidi elfu moja waweka silaha chini katika sehemu ya Mahajah ya Homeh ya Deraa, kufuatia makubaliano ya suluhu yaliofanyika baina ya wakazi waliokuwa na silaha wa sehemu hiyo na serikali ya Syria, ambapo katika sehemu maisha ya kawaida ya wananchi hao yamerudi katika hali yake ya zamani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: watu elfu moja wameweka silaha chini sehemu ya Home ya Deraa nchini Syria, ikiwa ni katika kutekeleza suala la suluhu baina ya wananchi waliokuwa wameshika silaha katika sehemu hiyo na serikali ya nchi hiyo, kitu ambacho kimepelekea hali ya kawaida katika sehemu kurudi kama zamani.
Kwa mujibu Wwa ripoti hii, wawakilishi wa wakazi wa sehemu hiyo walifanya mazungumzo na wawakilishi wa Serikali hatimaye kusaini makubaliano ya suluhu kati ya vikundi viliokuwa na silaha na serikali ya nchi hiyo, ambapo muwakilishi wa serikali alikuwa ni kamanda “Wafiqi Nasir” ambaye ni mkuu wa masuala ya ulinzi na usalama katika maeneo ya kusini mwa Syria.
Sehemu ya Mahajah inawakazi wapatao elfu 23, ambapo mji wa Al-faqii uliopo mashariki mwa Mahajah ulishakuwa umekombolewa na majeshi ya Syria mnamo tarehe 10 mwezi Desemba mwaka 2016.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky