Magaidi wa Daesh waingia Iraq kutoka Syria

Magaidi wa Daesh waingia Iraq kutoka  Syria

Waziri wa ulinzi nchini Iraq amesisistiza kuwa wataongeza juhudi za kuongeza ulinzi katika maeneo ya mipaka iliopo magharibi mwa Anbar iliopakana na Syria

shirika la habari AhluLbayt (a.s) ABNA: Waziri wa ulinzi nchini Iraq amesisistiza kuwa wataongeza juhudi za kuongeza ulinzi katika maeneo ya mipaka iliopo magharibi mwa Anbar iliopakana na Syria.
wizaara hiyo imeongeza kusema kuwa: Magaidi wa Daesh wamekuwa wakiingia katika maeneo ya magharibi mwa Anbar na sehemu mbalimbali ziliopakana baina ya Syria na Iraq nakusababisha luondokewa na amani katika maeneo hayo.
kwa upande mwingine inasemekana kwamba kikundi cha kigaidi cha Daesh pamoja yakuwa kwa sasa hawamiliki eneo lolote katika  ardhi ya Iraq, ama kikundi hicho kimekuwa kinaonekana katika maeneo mbalimbali ya milima na majangwa nchini humo, jambo ambalo linapelekea kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa na hofu na kuhisi hatari.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky