Magaidi wa Syria walazimika kuondoka Quneitra

Magaidi wa Syria walazimika kuondoka Quneitra

Wapiganaji zaidi ya 2,800 ambao wanadhaminiwa na Israel wamekubali kuondoka mji wa mpakani wa Quneitra kufuatia kusalimu kwao amri chini ya makubaliano ya Urusi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wapiganaji zaidi ya  2,800 ambao wanadhaminiwa na Israel wamekubali kuondoka mji wa mpakani wa Quneitra kufuatia kusalimu kwao amri chini ya makubaliano ya Urusi.

Magaidi zaidi 2,800 wa Syria pamoja na familia zao wameondoka katika mkoa wa kusini magharibi mwa Quneitra jana, kuelekea mkoa wa kaskazini magharibi wa Idlib, kufuatia makubaliano mapya yaliyosimamiwa na Urusi.

Takriban mabasi 55 yaliondoka Quneitra yakiwa yamebeba kundi la kwanza la wapiganaji hao waliosalimu amri  katika eneo hilo.

Chini ya makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Urusi, waasi walikubali kuusalimisha kwa jeshi la Syria mkoa wa Quneitra ambao pia uko katika mpaka na milima ya Golan inayokaliwa na Israel. Pia walikubali kuzisalimisha silaha zao nzito.

Makubaliano kuhusu Quneitra ni ushindi mwingine muhimu kwa rais wa Syria Bashar al-Assad, ambaye katika miezi ya hivi karibuni, ameyakomboa maeneo mengi kusini mwa Syria akisaidiwa na wataalamu wa vita kutoka Iran.

Taarifa zinasema kuwa, makubaliano hayo hayakujumuisha kundi la wapiganaji wa kundi la kigaidi la Hayat Tahrir al-Sham.

Huku hayo yakijiri, kundi la uangalizi la haki za binadamu limesema ndege za kivita za Urusi zimeendelea kufanya mashambulizi makali katika maeneo yanayodhibitiwa na magaidi wa Khaled bin Walid ambaye ni mshirika wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu  magharibi mwa Deraa ambapo yote yanadhaminiwa na Israel na washirika wake.

Ndege hizo zililenga vijiji vya Heet na Taseel na kuwaua watu 26 wakiwemo watoto 11. Mapema siku ya Ijumaa, makubaliano ya kuwaondoa watu katika miji miwili inayoiunga mkono serikali lakini iliyozingirwa na waasi yalikamilishwa.

Rami Abdel Rahman ambaye ni mkuu wa shirika la uangalizi wa haki za buinadamu la Syria ameongea kuwa, makubaliano ya al-Foua na Kfarya yalitimizwa na mabasi yote yaliingia katika maeneo ya utawala, huku mamia ya wafungwa wa upinzani walioachiliwa huru wakiingia katika ngome za waasi.

Ameongeza kuwa waliohamishwa wameelekea katika makazi ya muda mfupi ya Jibreen karibu na mji wa Aleppo kaskazini mwa Syria.

Mnamo Alhamisi, tofauti iliibuka kuhusu wafungwa wa upinzani walioshikilia mabasi 23 yaliyowabeba watu kutoka vijiji viwili vinavyounga mkono serikali karibu na kivukio cha Ays katika vijiji vya Aleppo.

Tofauti hiyo ilitokea pale waasi walilalamika kuwa baadhi ya hao walioachiliwa walikuwa wafungwa waliokamatwa hivi karibuni na utawala ulioko madarakani na si wanachama wa kundi la Al-Qaeda linalohusishwa na Hayat Tahrir al_Sham lilivizingira vijiji viwli vinavyopendelea serikali.

Kwa mujibu wa kundi la uangalizi la haki za binadamu, takriban mabasi 120 yamewabeba watu 6,900 kutoka vijiji vinavyounga mkono serikali.

Wakati hayo yanajiri Israel ambayo ni mdhamini mkubwa wa makundi hayo ya kigaidi, imekuwaikikosa  usingizi kufuatia majeshi ya Iran kuzidi kusogea karibu na mipaka ya taifa hilo.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky