Magaidi watano wa Daesh wakamatwa na majeshi ya Lebanon nchini humo

Magaidi watano wa Daesh wakamatwa na majeshi ya Lebanon nchini humo

Majeshi ya Lebanon siku ya Jumatano ya leo wamefanikiwa kuwakamata magaidi watano wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika sehemu ya “Mashariul Alqaa” ambapo ni karibu na mipaka ya Syria na nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kukamatwa kwa magaidi watano wa Daesh zasambazwa katika vyombo vya habari vya Lebanon.

Majeshi ya Lebanon siku ya Jumanne ya leo wamefanikiwa kuwakamata magaidi watano wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika sehemu ya “Mashariul Alqaa” ambapo ni karibu na mipaka ya Syria na nchi hiyo.

Kukamatwa kwa magaiadi hao ni baada ya majeshi ya Lebanon kwenda kufanya uchunguzi katika kambi ya wakimbizi wa Syria, ambapo baada ya kukamatwa kwao wameamishwa kutoka sehemu hiyo na kupelekwa katika kambi za majeshi ya Lebanon kwaajili ya kuojiwa zaidi.

Kikundi cha kigaidi cha Daesh jana kilishambulia ardhi ya Lebanon kwa makombora saba, ama kwa bahati nzuri hakuna yeyote aliyepoteza maisha kufuatia mashambulio hayo.

Vyombo vya ulisnzi nchini Lebanon jana kimefanikiwa kumkamata gaidi mmoja wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ambaye ni mwananchi wa Syria katika mji mkuu wa nchi hiyo, ambapo alikuwa anaamia katika kambi ya wakimbizi wa Palestina nchini humo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky