Magaidi wawili wa Daesh waangamizwa kaskazini mwa mashariki ya Diyala

Magaidi wawili wa Daesh waangamizwa kaskazini mwa mashariki ya Diyala

Wawi kati ya magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ambao walikuwa wakitaka kujiripua, baada ya kuzingirwa na majeshi ya usalama ya Iraq sehemu ya Al-hafayir kaskazini mwa mashariki mwa mkoa wa Diyala nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:kiongozi mmoja wa mkoa wa Dayala nchini Iraq ametangaza kuwa magaidi wawili wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ambao walikuwa na lengo la kujiripua wameangamizwa baada ya kuzingirwa na majeshi ya Iraq sehemu ya Al-hafayer iliopo katika mkoa wa Dayala.
Msimamizi mkuu wa kamati ya Miqdadiyah iliopo katika mkoa wa Dayala amesema:kufuatia mashambulizi ya kuwasambaratisha magaidi waliopo sehemu ya Al-hafayer iliopo karibu Talal Hamrin msahariki ya Al-miqdadiyah, ambapo majeshi ya ulinzi na usalama ya Iraq waliwazingira magaidi wawili waliokuwa katika nyumba mbovu ambao walikuwa wamejivika mabomu tayari kwa kwaajili ya kufanya tukio la kigaidi na baada ya kuwazingira na kutokea mashambulio baina yao mwisho waliangamia magaidi hao.
Aidha ameongeza kusema kuwa: mashambulio hayo yalifanyika kwa majibu wa ratiba iliokuwa imepangwa toka mwanzo na majeshi ya ulinzi na usalama katika sehemu hiyo, pia jana majeshi ya usalama ya Iraq katika mkoa wa Diyala na kufanikiwa kuwasambaratisha magaidi kadhaa wa kikundi cha kigaid katika sehemu hiyo.
Inasemekana kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, baada yakuwa wamesambaratishwa katika maeneo waliokuwa wameyateka, wamekimbilia nje ya miji ya mikoa hiyo ambapo wanaishi katika milima na baadhi ya nyakati huja katika maeneo wanayoishi watu wa kawada na kufanya mauaji kwa wanajeshi na wananchi.
Majeshi ya usalama ya Iraq katika mikoa mbalimbali nchini humo, hufanya mashambulizi kwaajili ya kusambaratisha mabakia ya magaidi waliobaki katika sehemu hizo.    
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky