Magaidi wawili wa Daesh waangamizwa katika mapando na Polisi wa Indonesia

Magaidi wawili wa Daesh waangamizwa katika mapando na Polisi wa Indonesia

Polisi wa kupambana na ugaidi nchini Indonesia wametangaza kuwaangamiza magaidi wawili ambao wanadaiwa kuwa wanamawasiliano na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:  Polisi wa kupambana na ugaidi nchini Indonesia wametangaza kuangamia kwa magaidi wawili ambao wanadaiwa kuwa wanamawasiliano na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Magaidi hao wawili walikuwepo katika kisiwa cha Sumbawa ambapo baada ya mapambano makali na majeshi ya usalama ya nchi hiyo waliuliwa katika kisiwa hicho.
Mapambano na magaidi hao yalianza kipindi ambacho majeshi ya usalama ya kupambana na ugaidi nchini Indonesia yalikuwa katika mji wa Bima wakifanya dolia ya kuwasaka magaidi hao, walipowakuta ndipo yakaanza mashambulizi na magaidi hao, mwisho wa mashambulizi hao kulipelekea kuangamia magaidi wawili na wengine kufanikiwa kukimbia sehemu hiyo.
Inasemekana kuwa Indonesia kunakikundi cha kigaidi cha Ansaru Dawlah ambacho kinafungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo serikali ya Indonesia inajitahadi kukabiliana na kikundi hicho.    
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky