Magaii wa Daesh wauwa wanajeshi 25 wa Kikurdi nchini Syria

Magaii wa Daesh wauwa wanajeshi 25 wa Kikurdi nchini Syria

Kikundi cha kigaidi cha Daesh kilifanya mashambuio makali dhidi ya majeshi ya wakurdi nchini na kuuwa wanajeshi 25 nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimefanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya Wakurdi katika mkoa wa Deirrz-zor nchini Syria na kupelekea kuuwawa wanajeshi 25 na wengine 35 kufanya mateka.
Magaidi wa Daesh katika shambulio hilo, walitumia vizuri fursa ya hali mbaya ya hewa iliokuwa katika maeneo yanayokaliwa na wakurdi nchini humo, ambapo kulitokea kimbunga kikali kilichokuwa kimesambaza vumbi kali katika maeneo hayo na kuweza kufanikiwa katika jambo lao.
Aidha kikundi cha kigaidi cha Daesh kifanya mashambulizi katika sehemu mbalimbali zinazokaliwa na Wakurdi nchini Syria na kufanya jinai mbalimbali katika sehemu hizo, Ama katika shambulio hili wameuwa wanajeshi 25 wa Kikurdi na wengine 35 kutekwa nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky