Majeshi ya Israel yashambulia Meli ya Gaza na kuwateka waliokuwa katika meli hiyo

Majeshi ya Israel yashambulia Meli ya Gaza na kuwateka waliokuwa katika meli hiyo

Mitumbwi kadhaa ya majeshi ya utawala haramu wa Israel yashambulia Meli ya Wapalestina wa ukanda wa Gaza iliokuwa inalengo la kutoka katika masafa yalioanishwa na utawala haramu wa Israel katika ukanda wa Gaza na kuwateka Wapalestina wote waliokuwa katika Meli hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msemaji wa vyombo vya habri vya Palestina ametangaza kuwa mitumbwi mine ya majeshi ya kivamizi ya Israel yalishambulia Meli aliokuwa na wapalestina hatuimaye kuizingira na kuwateka wote waliokuwa katika Meli hiyo.
Hayo yamesemwa na “Adhami Abu-Sulaimah” akibainisha kuwa Meli hiyo ilibeba apalestina 20, ikiwemo wagonjwa na wanafunzi ambapo walikuwa wanakwenda Cyprus kwaajili ya matibabu na wengine kujiendeleza kimasomo.
Aidha ameongeza kusema kuwa: majeshi ya maji ya utawala haramu wa Israel baada ya kuiteka Meli hiyo wameifikisha katika Bandari ya Ashdod katika maeneo yanayokaliwa na kimabavu na utawala haramu wa Israel.
La muhimu kuashiriwa ni kwamba mpaka ni miaka 12 ukanda wa Gaza umezingirwa na majeshi ya Kizayuni kwa maana wakazi wa sehemu hawaruhusiwi kutoka kwenda sehemu yeyote, huku maelezo yanasema kuwa utwala wa Kizayuni huzuia Mitumbwi ya Wapalestina kutoka nje ya ufukwe kwa umbali wa maili moja, hata mitubwi ya wavuvi pia huzuiliwa kwenda zaidi ya umbali huo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky