Majeshi ya Marekani yapungua nchini Iraq baada ya Daesh kushindwa nchini humo

Majeshi ya Marekani yapungua nchini Iraq baada ya Daesh kushindwa nchini humo

Msemaji mkuu wa serikali ya Iraq ametangaza kupungua kwa majeshi ya Marekani nchini humo, baada ya Iraq kutangaza kusambaratika kwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msemaji wa serikali ya Iraq ametangaza kupungua kwa majeshi ya Marekani nchini humo baada ya serikali hiyo kutangza mwisho wa kuwepo kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Aidha Saad Al-hadithiy ameongeza kusema kuwa, baada ya kusambaratika kwa kikundi cha kigaidi Daesh, majeshi ya Marekani yameonekana kuanza kupungua katika ardhi ya taifa hilo.
Kundi la wanajeshi kadhaa wa majeshi ya Marekani nchini Iraq, wika iliopita wameondoka nchini humo na kuelekea nchini Afghanistan wakiwa pamoja na vifaa vyao vya kivita, inavyoonekana wamarekani wamekili kunako suala la kuondoka nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky