Majeshi ya Syria yakomboa mji wa Deir ez-Zor nchini Syria

Majeshi ya Syria yakomboa mji wa Deir ez-Zor nchini Syria

Kikundi cha jumuia ya haki za binadamu nchini Syria ambao wanawaunga mkono wanaoipinga serikali ya Syria, wamesema kuwa majeshi ya Syria yamefanikiwa kuikomboa makao makuu ya mji wa Deir ez-Zor kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaid cha Daesh

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kikundi cha jumuia ya haki za binadamu nchini Syria ambao wanawaunga mkono wanaoipinga serikali ya Syria, wamesema kuwa majeshi ya Syria yamefanikiwa kuikomboa makao makuu ya mji wa Deir ez-Zor kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Makao makuu ya utoaji wa habari za vita imetangaza kukombolewa kwa sehemu ya Al-hamdiyah iliopo katika mji wa Deir ez-Zor nchini humo.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo yameelezea azma ya majeshi ya Syria na washirika wake ya kumaliza haraka mashambulio ya kuukomboa mji wa Deir ez-Zor, huku wakisisitiza kuwa  usiku wa Alhamisi umeshasafishwa mji huo kikamilifu. Ama majeshi ya Syria kwa upande wake mpaka sasa halijatangaza lolote kuhusu habari hizo.
Majeshi ya Syria yametangaza kufanikiwa kukomboa maeneo kadhaa yaliopo katika mji wa Deir ez-Zor ikiwemo sehemu ya “Al-jubailiyah), “Al-Jamiyati” ikiwemo ni sehemu ya mji wa Deir ez-Zor.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky