Majeshi ya Syria yakomboa sehemu ya milima ya Al-Shumariyah

 Majeshi ya Syria yakomboa sehemu ya milima ya Al-Shumariyah

Majeshi ya serikali ya Syria yamefanikiwa kukomboa sehemu ya miinuko ya Al-Shumariyah iliopo katika Homeh ya mashariki ya mkoa wa Homs, kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya serikali ya Syria kwa mara nyingine tena wafikia ushindi dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Majeshi hayo siku ya Jumatano ya tarehe 3 mwezi watano, wamefanikiwa kuikomboa sehemu ya miinuko ya Al-Shumariyah iliopo Homeh ya mashariki ya mkoa wa Homs kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Ushindi huo umefikiwa katka mashmabulizi yaliofanyika katika sehemu hiyo iliokuwa na urefu wa kilometa 13 na upana wa kilometa 9 mashariki mwa mji wa Homs, ambapo katika mashambulio hayo makumi ya magaidi wa Daesh wameangamia na wengine wengi kujeruhiwa.
Aidha majeshi ya Syria pia yamefanya mashambulio katika ngome za kikundi cha kigaidi cha Daeh katika sehemu mbalimbali ya mashariki mwa Homs, ambapo magari ya kijeshi ya kikundo hicho pia yameangamizwa huku magaidi 6 wa kikundi hicho kuangamia katika sehemu hiyo.
Majeshi ya Syria toka siku kadhaa ziliopita yalianza mashambulizi makali kwaajili ya kuikomboa sehemu ya Homeh ya mashariki ya mkoa wa Homs kutoka kwa vikundi vya kigaidi vya Daesh, ambapo kufuatia mashmabulio hayo vijiji kadhaa vya mkoa wa Homs ambavyo vilikuwa chini ya vikundi vya kigaidi kukombolewa.
Mji wa Homs hivi sasa uko chini ya majeshi ya Syria, ama vikundi vya kigaidi vya Daesh vipo katika maeneo ya Homeh ya mashariki ya mji huo nchini Syria.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky