Majeshi ya Syria yakomboa vijiji 24 sehemu ya Humeh ya Adlib

Majeshi ya Syria yakomboa vijiji 24 sehemu ya Humeh ya Adlib

Vikosi vya majeshi ya Syria yamefanikiwa kukomboa vijiji 24 viliopo katika mkoa wa Adlib, baada ya mapambano makali kati ya majeshi hayo na kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya ulinzi na uasalama ya Urusi leo imetangaza kuwa, vikosi vya majeshi ya Syria yamefanikiwa kukomboa vijiji 24 nchini humo baada ya mapambano makali katika ya majeshi ya Syria na kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah katika maeneo ya mkoa wa Adlib.
Aidha majeshi ya Syria yamekuwa yakisonga mbele kuelekea uanja wa ndege wa Abudhuhri, ambapo zimebaki kilometa tano mpaka kufika katika uwanja huo, huku wakifanikiwa kuwazingira magaidi 1500 wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky