Mamia ya wakimbizi wa Syria warudi nchini mwao kutoka Lebanon

Mamia ya wakimbizi wa Syria warudi nchini mwao kutoka Lebanon

Kundi lingine la wakimbizi wa Syria waliokuwa nchini Lebanon wamefanikiwa kurudi katika makazi yao nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kundi lingine la wakimbizi wa Syria waliokuwa nchini Lebanon wamefanikiwa kurudi katika makazi yao nchini Syria.
Aisha wakimbizi hao walikusaniyika katika mji wa Shabaa uliopo kusini mwa Lebanon na wakapanda magari yalio andaliwa kuwafikisha katika sehemu ya Buqaa iliopo katika mipaka ya Syria na Lebano, wakimbizi hao ambao kwa uchache walikuwa 200 walivuka katika boda za nchi hiyo na kuingia nchini Syria.
Inasemekana ni kwamba wakimbizi zaidi ya milioni moja na nusu ambao ni wananchi wa Syria wapo nchini Lebanon, ambapo viongozi wa Lebanon kutokana na atahari za kiuchumi na usalama zinazo sababishwa na kuwepo kwa idadi hiyo, waliomba kurejeshwa baadhi ya wakimbizi katika makazi yao ambayo kwamba muda mrefu yalishakuwa yamepata amani na utulivu.
Hivi sasa serikali ya Syria imeanza juhudi kubwa ya kupeleka huduma za msingi na kutengeza miundombinu ya barabara, mfumo wa umeme, maji na kutengeza vituo vya afya katika sehemu mbalimbali yaliokombolewa kutoka kwa magaidi ikiwa ni sehemu ya kuandaa mazingira ya kurudi wakimbizi wote waliokuwa katika sehemu mbalimbali katika mataifa mengine.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky