Maulamaa 300 wa Kiislamu watangaza kuwa haramu uhusiano na Israel

Maulamaa 300 wa Kiislamu watangaza kuwa haramu uhusiano na Israel

Maulamaa wapatao 300 wa Kiislamu wamekutana Istanbul Uturuki na kutangaza kuwa uhusiano wowote wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ni haramu.

Maulamaa hao ambao walikuwa wakiwakilisha jumuiya na taasisi 36 za Kiislamu kutoka maeneo yote duniani wamewahutubia waandishi habari  baada ya kikao chao wiki hii na kutia saini ‘Hati ya Maulamaa wa Umma wa Kiislamu”  ambapo wamebainisha wazi kuwa haramu uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Washiriki wa kikao hicho wamesisitiza kwamba, kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ni hatari kwa harakati za ukombozi wa Palestina huku wakitoa wito kwa Waislamu kuususia utawala huo ghasibu.

‘Hati ya Maulamaa wa Umma wa Kiislamu’ ina vipengee 44 na moja kati ya sehemu zake muhimu inahusu msimamo wa Kiislamu kuhusu utawala wa Kizayuni.

Hivi karibuni pia Sheikh Mkuu wa al Azhar ya Misri alitahadharisha kuhusu taathira za uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua rasmi mji mtakatifu wa Quds kuwa eti ni mji mkuu wa utawala bandia wa Israel na kutaka kufanyika mkutano wa kimataifa wa kujadili suala hilo.

Sheikh Ahmad al Tayyib alisema kuwa uamuzi huo wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Quds unaamisha kukanyagwa haki za Wapalestina na Waarabu katika mji wa Quds na kupuuzwa matukufu ya Waislamu na Wakristo. Sheikh al Tayyib amewataka maulamaa wa ngazi za juu wa al Azhar kuitisha kikao cha dharura kuchunguza athari za uamuzi huo wa Trump.  
................
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky