Mfalme wa Bahrain aliridhishwa na mitazamo mipya ya Trump dhidi ya Iran

Mfalme wa Bahrain aliridhishwa na mitazamo mipya ya Trump dhidi ya Iran

Serikali ya Bahrain baada ya utawala haramu wa Israel na Saudi Arabia kuunga mkono mitazamo ya serikali ya Marekani, nalo limekuwa taifa la tatu lilionga mkono mitazamo mipya ya Trump dhidi ya serikali ya kiislamu ya Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: serikali ya kifamle ya Bahrain na umoja wa Falme za kiarabu zimeungana na mataifa yanayounga mkono mitazamo ya Rais wa Marekani dhidi ya serikali ya Iran.
Utawala wa Bahrain usiku wa Ijumaa ulitangaza kuwa serikali hiyo inaunga mkono mitazamo mipya ya Donald Trump Raisi wa Marekani dhidi ya serikali ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Aidha Bahrain imeunga mkono mitazamo hiyo baada ya wakuu wake (saudi Arabia) kukubaliana na mitazamu hiyo, ilidai kuwa Iran inaunga mkono vikundi vya kigaidi duniani, huku wakisistiza kuwa serikali ya Bahrain inaunga mkono kila juhudi za kuizuia Iran katika suala hilo.
Kadhalika serikali ya Bahrain imedai kuwa, jeshi la kulinda mapinduzi ya kiislamu ya Iran ni lakigaidi nakusema kuwa serikali ya Bahrain imepata madhara makubwa kutoka kwa jeshi hilo.
Wizara ya mambo ya nje ya serikali ya Falme za Kiarabu nayo imeunga mkono mitazamo mipya ya serikali ya Marekani na kudai kuwa siasa za serikali ya Iran katika ukanda wa mashariki ya kati ni siasa mbaya, ambapo serikali ya umoja wa Falme za Kiarabu inashirikiana na Marekani na washirika wake katika kukabiliana na serikali ya Iran.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
We are All Zakzaky