Mji mkuu wa Saudi Arabia washambuliwa na mabomu ya Yemen

Mji mkuu wa Saudi Arabia washambuliwa na mabomu ya Yemen

Vyombo vya habari mbalimbali vyatangaza kushambuliwa kwa makombora ya Yemen katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Saudi Arabia wametangaza kuwa, usiku wa Jumapili kulisikika sauti kadhaa za milipuko katika mji mkuu wa Saudi Arabia.
Aidha kikusi cha makombora katika majeshi ya Yemen na Ansarullah wametangaza kushambulia makao makuu ya wizara ulinzi na usalama nchini Saudi Arabia, pia kituo kingine kikubwa katika mji wa Riyadh kwa makombora kadhaa ya kisasa nchini humo.
Kwa upande mwingine Televishen ya Al-arabia, imetangaza na kudai kuwa vifaa vya kijeshi vya kulinda anga nchini Saudi Arabia vimeangamiza makombora yaliokuwa yamerushwa kutoka Yemen kabla ya kufika katika sehemu iliokuwa imelengwa.
Msemaji mkuu wa vikosi vya uvamizi nchini Yemen kwa usimamizi wa Saudi Arabia, wiki iliopita amekiri kuwa mpaka sasa makombora zaidi ya 149 ya Yemen yameshambulia nchini Saudi Arabia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky