Mmoja kati ya makamanda wa ngazi zajuu wa Saudia apoteza maisha

 Mmoja kati ya makamanda wa ngazi zajuu wa Saudia apoteza maisha

Kamanda “Mithali Hizaa Abu-hulaybah Ad-dihaniy” katika makamanda wa jeshi namba sita la Saudi Arabia amekufa kufuatia mapambano makali yaliotokea baina ya majeshi ya Saudi Arabia na Yemen

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Yemen vimetangaza kuangamia kwa kamanda Mithali Hizaa Abu-hulaybah Ad-dihaniy” ambaye ni katika makamanda wa ngazi za juu wa jeshi namba sita la Saudi Arabia katika mapambano yaliotokea baina ya majeshi ya Yemen na Saudi Arabia.
Baadhi ya Vyombo vya habari vikinukuu kutoka kwa vyanzo vya Saudi Arabia vimetangaza kuwa Ad-dihaniy alijeruhiwa katika mapambana na majeshi ya Yemen katika sehemu ya Najiran na baada ya hapo alipoteza maisha.
Vyombo vya habari vya Yemen pia vimetangaza kuwa: wanajeshi wengine 8 pia wamekufa pamoja naye baada ya kuingia katika mtego uliotegwa na majeshi ya Yemen.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky