Mtawala wa Daesh katika mji wa Diyala aangamizwa

Mtawala wa Daesh katika mji wa Diyala aangamizwa

Kamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mkoa wa Diyala ameangamia kufuatia shambulio la anga liliofanywa na majeshi ya Iraq katika sehemu ya Baqubah

Shirika la habari Ahlulabayt (a.s) ABNA: msimamizi mkuu wa mashambulizi dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mkoa wa Diyala amesema: Kamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mkoa wa Diyala ameangamia kufuatia shambulio la anga liliofanywa na majeshi ya Iraq katika sehemu ya Baqubah.
Aidha Mudhihir Al-azawiy ameongeza kusema kuwa: kamanda huyo wa Daesh aliokuwa na jina Riyadh, pamojana msaidizi wake, ameangamia kufuatia shambulio la anga liliofanywa na majeshi ya Iraq katika sehemu ya Alkhalawiyah kaskazini mwa Baqubah.
Pia amemaliza kusema kuwa: kufuatia mashambulio ya anga yaliofanywa na majeshi ya Iraq, yamesababisha kuangamia kwa makamanda wengi wa kikundi cha kigaidi Daesh nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky