Amnesty International

Myanmar inaendeleza maangamizi ya kimbari dhidi ya Waislamu Warohingya

Myanmar inaendeleza maangamizi ya kimbari dhidi ya Waislamu Warohingya

Jeshi la Myanmar lingali linatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo kwa kutumia mbinu kadhaa.

Katika taarifa, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema jeshi la Myanmar linatumia mbinu kama njaa ya lazima, kueneza hofu kupitia utekaji nayara na pia uporaji mali ili kuwalazimu Waislamu waondoke katika ardhi zao za jadi katika jimbo la Rakhine.

Amnesty imesema mbinu hizo za maangamizi ya kimbari zingali zinaendelea hata baada ya Myanmar kutia saini mapatano nan chi jirani ya Bangladesh kuhusukurejeshwa wakimbizi zaidi ya 700,000 Waroghinya ambao walipata hifadhi katika nchi hiyo baada ya kuanza wimbi jipya la mauaji ya kimbari mwezi Agosti.

Hayo yanajiri wakati ambao makaburi ya umati ya Waislamu waliouawa nchini Myanmar yamepatikana katika kijiji kimoja katika jimbo la Rakhine magharibi mwa nchi hiyo.

Jinai kubwa wanazofanyiwa Waislamu hao na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo  wenye misimamo ya kufurutu katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa Myanmar zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu. Hadii sasa  jina hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu sita na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine karibu laki saba wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Zeid Ra'ad Al Hussein anasisitiza kwamba, kuna udharura wa kufika katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kufanya uchunguzi kuhusu ukatili unaofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu.
..........
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky