Saudi arabia yawazuia wananchi wa Syria kushiriki ibada ya Hija

Saudi arabia yawazuia wananchi wa Syria kushiriki ibada ya Hija

Serikali ya Saudia Arabia mwaka huu pia imewazuia wananchi wa Syria kushiriki katika ibada mujimu ya Hija

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya Waqfu na masuala na ibada ya Hija nchini Syria imetoa tangazo rasmi kuwa, serikalii ya Saudi Arabia mwaka huu kwa mara nyingine ukiwa mwaka wa saba yawazuia wananchi wa Syria kushiriki katika ibada ya Hija nchini humo.
Wizara ya hiyo imebainisha suala hilo na kuongezea kuwa: suala la kutekeleza ibada ya Hija limefanywa kuwa lakisiasa kupitia serikali ya Saudi Arabia jambo ambalo limeifanya Syria isiruhusiwe kushiriki katika ibada hiyo kwa muda wa miaka saba ukijumuisha na mwaka huu.
Aidha wizara hiyo imebanisha kuwa: maranyingi imejaribu kupitia jumuia ya umoja wa nchi za kiislamu kwaajili ya kuitaka Saudi Arabia itowe ruhusa kwa wananchi wa Syria kushiriki katika ibada ya Hija, ama bila ya mafanikio, pia katika imeelezwa kuwa: ibada ya Hija imegeuzwa na kutumika  katika masuala ya kisiasa.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky