UNICEF: watoto milioni 12 nchini Yemen wanahaja msaada wa haraka

UNICEF: watoto milioni 12 nchini Yemen wanahaja msaada wa haraka

UNICEF imeyasema hayo na kutangaza kuwa: katika maeneo mbalimbali nchini Yemen watoto zaidi ya milioni 11 wanahitaji msaada wa kibinadamu wa haraka zaidi hususan msaada wa vyakula

Shirika la habari AhluLbayt (a.s) ABNA: shirika la misaada kwa watoto katika umoja wa mataifa (UNICEF) limetoa kauli hiyo na kuzitaka pande mbili ziliokuwa na uhasama kutumia njia ya mazungumzo ya kisiasa badala ya mapigano ya kivita.
Msimamizi wa masuala ya jumuia hiyo amebainisha kuwa mapigano ya pande mbili hizo nchini Yemen imekuwa ni sababu inayopelekea kusambaratika kwa nchi hiyo na kuharibu miundombinu ya uchumi na huduma za kijamii nchini humo.
Aidha amebanisha kuwa: bei za bidha nchini humo zimepanda kwa kiasi kikubwa, Hospitali zimeharibiwa, sehemu za mafunzo zimebadirika kuwa ndio maficho ya wakimbizi au zimetekwa na vikundi viliokuwa na silaha, katika hali hiyo UNICEF inafanya juhudi ya kuwasaidia vijana na watoto walio athirika nchini humo, huku tukitoa ushauri wa kutumika njia ya mazungumzo katika kutatua mgogoro wa Yemen.
Katika maelezo ya kiongozi huyo imeelezwa kwamba katika sehemu mbalimbali nchini Yemen kuna watoto zaidi ya milioni 11 wako katika hali hatarishi ambapo wanahitaji msaada wa kibinadamu kwa haraka zaidi hususan vyakula na maji ya kunywa.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky