Urusi: wakimbizi 1000 warejea katika makazi yao nchini Syria

Urusi: wakimbizi 1000 warejea katika makazi yao nchini Syria

Makao makuu ya kuwahudumia wakimbizi nchini Urusi imetangaza kuwa wakimbizi zaidi ya elfu moja wamerudi katika makazi yao mnamo masaa 24 yalioipita

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Makao makuu ya kuwahudumia wakimbizi nchini Urusi imetangaza kuwa wakimbizi zaidi ya elfu moja wamerudi katika makazi yao mnamo masaa 24 yalioipita.
Makao makuu hayo katika ripoti yake emetangaza kuanzia kuanzia siku iliopita zaidi ya wakimbizi 1125 wamerejea katika makazi yao nchini Syria, ambapo watu 578 walikuwa nchini Lebanon na 547 ni kutoka nchini Jordan, vilevile 298 wametoka katika kambi za daima za wakimbizi ziliopo nchini Syria hatimaye kurejea katika makazi yao ya awali nchini humo.
Kurejea kwa wakimbizi wa Syria katika makazi yao ni ishara ya kukoma kwa vita ya miaka minane nchini humo, ambapo serikali ya Syria imefanikiwa kushinda katika vita hiyo dhidi ya vikundi vya kigaidi nchini humo, pamoja ya kuwa taifa hilo linahitaji uboreshaji mkubwa wa maundombinu katika maeneo yalioharibiwa kufuatia vita hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky