Vijana watu wa mapinduzi ya Bahrain wauwawa

Vijana watu wa mapinduzi ya Bahrain wauwawa

Vyombo vya usalama vya serikali ya Bahrain vimeuwa vijana watatu wa nchi hiyo katika bahari ya Ghuba ya uajemi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuuwawa kwa vijana watatu wa mapinduzi ya Bahrain zimetangazwa siku ya Alhamisi nchini humo
Vijana hao ni “Ridha al-Ghusra”, “Muhammad Yahya” na “Mustwafa Abdi Ali” ambapo wameuwawa katika bahari ya Ghuba ya Uajemi kupitia wana usalama wa utawala wa Ali Khalifah nchini humo.
Msimamizi wa vyombo vya usalama nchini Bahrain katika mahojiano yake na vyombo vya habari amedai kuwa wamefanikiwa kukabiliana na vijana wa mapinduzi ya Bahrain waliokuwa wanataka kukimbia katika bahari ya Ghuba ya Uajemi.
Aidha amesema majeshi ya kulinda mipaka ya nchi hiyo yalitoa amri ya kusimamisha mtumbwi mmoja katika bahari ya Ghuba ya Uajemi, ama baada ya waliopo katika mtumbwi huo kuto tii amri hiyo, wanajeshi wa Bahraini waliwafyatulia risasi na kupelekea kuuwawa kwa watu watatu waliokuwa katika mtumbwi huo.
Naye ameendelea kusema kuwa watu 7 wengine wamekamatwa kufuatia tukio hilo na watu wawili kati yao ni wamejeruhiwa, huku akibainisha kuwa umri wa vijana hao ni baina ya miaka 20 na 38.
Kwa upande mwingine wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano makubwa katika sehemu mbalimbali nchini humo wakipinga mauaji ya vjana hao watatu kupitia wanajeshi wa utawala wa Ali khalifa nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky