Vijiji 25 vyakombolewa/ makumi ya magaidi waangamizwa magharibi mwa Anbar

Vijiji 25 vyakombolewa/ makumi ya magaidi waangamizwa magharibi mwa Anbar

Msimamizi wa masuala ya ulinzi na usalama katika mji wa Hadithah leo ametangaza kukombolewa kwa vijiji 25 huku akibaishiria kuangamia kwa makumi ya magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mashambulizi ya kuikomboa magaharibi mwa Anbar nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Msimamizi wa masuala ya ulinzi na usalama katika mji wa Hadithah leo ametangaza kukombolewa kwa vijiji 25 huku akibaishiria kuangamia kwa makumi ya magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mashambulizi ya kuikomboa magaharibi mwa Anbar nchini Iraq
Hayo yamesemwa na Mabruk Al-jughaifiy na kusisitiza kuwa majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuvikomboa vijiji 25 karibu na sehemu ya Al-qaim, huku akiashiria kuwa mashambulizi ya kuikomboa sehemu ya Al-qaim bado yanaendelea na kwa uwezo wa mwenyezi Mungu mwishoni mwa wiki itakuwa imeshakombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.
Mwesho ameeleza kuwa majeshi ya ulinzi na usalama ya Iraq yamewaangamiza makumi ya magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh na kuangamiza magari kadhaa ya kijeshi ya kikundi hicho.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky