Waliokufa kwa ugongwa wa kipindupindu nchini Yemen wafikia 2151

Waliokufa kwa ugongwa wa kipindupindu nchini Yemen wafikia 2151

Shiririka la afya duniani limetangaza kuendelea kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen, ambapo tokea kuanza kwa ugunjwa huo mpaka sasa watu 2151 wamepoteza maisha nchini humo

Shirika la habari AhlulalBayt (a.s) ABNA: shirika la afya duniani limetoa kauli yake mpya na kusema kwa ujumla watu laki 8 na 626 katika mikoa 22 miongoni mwa mikoa yote 23 wamepatwa na ugunjwa wa kipindupindu.
Idadi ya watu waliofariki kwa ugonjwa huo ukilinganisha hile iliotolewa awali, inaonyesha kuwa watu 24 wameongezeka katika idadi hiyo, hii ni katika hali amabyo ripoti zinaonyesha kuwa watu laki 3 na 102 ni idadi iliongezeka ya waliopatwa na ugonjwa huo nchini Yemen.
Mkoa ulikuwa umeathirika zaidi ni mkoa wa Hajeh ulipo kaskazini mwa nchi hiyo, huku ikielezwa kuwa mkoa ulioathirika zaidi ni mkoa wa Hadideh kaskazini mwa magharibi mwa Yemen katika kingo ya bahari ya nyekundu.
Jumuia ya kimataifa ya msaraba mwekundu wiki iliopita ilitabiri kuongezeka kwa kuenea kwa ugonjwa huo mpaka ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, watu watakaopatwa na ugonjwa huo watafika watu milioni moja.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky