Kikosi cha wadunguaji wa majeshi ya Yemen wamefanikiwa kuwauwa wanajeshi 4 wa majeshi yanayo fungamana na majeshi ya umoja wa kuivamia Yemen chini ya usimamizi wa Saudi Arabia kusini mwa Yemen
Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikosi cha masnaipa wa Yemen leo Jumatano wamefanikiwa kuangamiza wanajeshi wanne wa umoja wa kuivamia Yemen chini ya usimamizi wa Saudi Arabia katika sehemu ya Jizani kusini mwa Saudi Arabia.
Chanzo kimoja cha kijeshi nchini Yemen kimetangaza kuwa mamluki wa Saudi Arabia wamekuwa wakishambuia miinuko ya Ad-dud iliopo sehemu ya Jizani nchini humo, ambapo wadunguaji wa Yemen katika masiku ya hivi mwishoni wamefanikiwa kufanya mawindo katika maeneo mbalimbali ya sehemu hizo.
Aidha vyombo vya habari vya Yemen pia vimetangaza kuwa kufuatia mashambuliai yaliofanywa na masnaipa wao katika masaa 48 yaliopita wamefanikiwa kuwasambaratisha zaidi ya watu 4 na wengine kujeruhiwa katika mashambulio hayo ambapo kwa ujumla ni watu 44 waliouliwa na kujeruhiwa.
mwisho/290