Wanajeshi 6 wa Saudi Arabia waangamia katika mashambulizi ya majeshi ya Yemen

Wanajeshi 6 wa Saudi Arabia waangamia katika mashambulizi ya majeshi ya Yemen

Hayo yametokea kufuatia mashmbulizi ya majeshi ya Yemen dhidi ya majeshi ya Saudi Arabia yaliotokea baina ya mipaka wa Saudi Arabia na Yemen nakupelekea kuangamia kwa wanajeshi sita wa Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wapiganaji wa majeshi ya Yemen katika mashambulizi maalumu wamefanikiwa kuwaangamiza wanajeshi watatu wa Saudi Arabia katika sehemu moja inayoitwa Hamidh katika mkloa wa Jizani, pia mwanajeshi mwingine wa Saudi Arabia amepigwa risasi katika kambi ya kijeshi ya Ashah iliopo katika sehemu ya Najran nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa ripoti hii, majeshi ya usalama ya Yemen yakishirikiana na majeshi ya kujitolea wananchi nchini humo yamefanya mashambulizi maalumu ya kushambulia sehemu mbalimbali waliopo majeshi ya Saudi Arabia, ambapo yalifanywa sehemu ya Qais iliopo katika mkoa wa Jizani na vilevile kufanikiwa kuwaangamiza wanajeshi wawili wa Saudi Arabia na kufanikiwa kuwateka wanajeshi wanne wanaofungamana na majeshi ya utawala wa kivamizi wa Saudi Arabia.
Umoja wa waarabu chini ya usimamizi wa Saudi Arabia miaka miwili iliopita waliivamia kijeshi Yemen kwa madai ya kumsaidia Abdirabih Mansur Alahadiy, Rais alikuwa amiuzuru na kuondoka nchini Yemen, ambapo toka uanze uvamizi huo mpaka sasa imepelekea kuuwawa kwa maelfu ya watu na webgine wengi kujeruhiwa kufuatioa uvamizi huo.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky