wanajeshi 65 wa Saudi Arabia watekwa na majeshi ya Yemen

wanajeshi 65 wa Saudi Arabia watekwa na majeshi ya Yemen

majeshio ya Yemen kufuatia mashambulizi makali yaliofanyika katika mkoa wa Dhaliu wamefanikiwa kuwateka mamluki 64 wa majeshi ya Saudi Arabia

shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi imerusha makombora kadhaa katika maeneo mbalimbali waliopo mamluki wa Saudi Arabia katika sehemu ya Sharihah kaskazini mwa mkoa wa Lahaj na kusababisha kufa na kujeruhiwa idadi kubwa ya mamluki wa majeshi ya Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa ripoti hii na ripoti nyingine ziliotufikia ni kwamba, majeshi ya Yemen katika wiki moja iliopita wamefanikiwa kuwateka mamluki 65 wa majeshi ya Saudi Arabia katika mji wa Damat na Jubun iliopo katika mkoa wa Dhalii watu ambao walikamatwa kabla ya kufanya tukio la kigaidi waliopanga kulifanya katika maeneo hayo.
Katika hiyo pia majeshi ya Yemen yamefanikiwa kusambaratisha mashambulio makubwa mawili ya kigaidi waliotaka kuyafanya mamluki hao katika mji wa Tukhyata uliopo kusini mwa mkoa wa Hudaidah na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi 28 na wengine 21 kuwajeruhi na kuyaangamiza magari 10 ya kijeshi ya magaidi hao.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky