Watoto 27 waokolewa kutoka mikononi mwa kikundi cha Daesh

Watoto 27 waokolewa kutoka mikononi mwa kikundi cha Daesh

Msimamizi wa mambo ya waumini wa Izadi katika jamii ya Kikurdi nchini Iraq, ametangza kukombolewa kwa watu 37 walikuwa wametekwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh ikiwemo watoto 27.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kukombolewa kwa watu kadhaa waliokuwa wametekwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambao ni wafuasi wa dhehebu la Izadiy zimetangazawa nchini humo.
Msimamizi wa mambo ya wafuasi wa madhehebu ya Izadi katika jamii ya Wakurdi ametangaza kukombolewa kwa watu 37 wa dhehebu la Izadi ikiwemo watoto 27 kutoka kwa kikundi hicho, ambapo inasadikiwa kuwa mateka hao wote ni wakazi wa sehemu ya Sinjari nchini humo.
Kwa mujibu wa takwimu ya msimamizi wa mambo ya wafuasi wa Izadi, mpaka sasa zaidi ya watu elfu 2 na 900 waliokuwa wametekwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh, wamekombolewa na majeshi ya Iraq, katika hali ambayo takriban waizadi wengine wengi bado wako mikononi mwa kikundi hicho cha kigaidi.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh mnamo mwaka 2014 walifanya mashambulizi ya kigaidi katika maeneo yanayokaliwa na wafuasi wa madhehebu ya Izadi katika mji wa  Sinjar mkoani Nineveh kaskazini mwa Iraq, ambapo kufuatia mashambulizi hayo mamia ya wakazi wa sehemu hiyo wamepoteza maisha na asilimia kubwa ya wakazi hao kutekwa na kikundi hicho.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh katika miaka ya hivi mwishoni waliwachukua baadhi ya watoto hao na kuwapeleka katika vituo vya mafunzo, ambapo baada ya kuchukua mafunzo ya itikadi na kijeshi, hujiunga na majeshi hayo na kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky