Watu 100 wafariki na kujeruhiwa katika mripuko wa kigaidi katika mkusanyiko wa wakimbizi wa Syria

Watu 100 wafariki na kujeruhiwa katika mripuko wa kigaidi katika mkusanyiko wa wakimbizi wa Syria

Mripuko wa kigaidi uliofanywa na magaidi wa kikundi cha Daesh watokea katika mkusanyiko wa wakimbizi waliokimbia katika mji wa Deir ez-Zor na kupelekea kuwawa na kujeruhiwa watu 100 katika tukio hilo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: tukio hilo limetokea baada ya gari liliokuwa limetegwa mabomu kuripoka baina wakimbizi walikuwa sehemu hiyo iliokuwa nje kidogo na mji wa Deir ez-Zor na kusababisha mauaji hayo.
Gari hilo liliokuwa limetegwa mabomu liliegeshwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika sehemu ya kukusanyika wakimbizi wanaotoka mji wa Deir ez-Zor mashariki mwa mto wa Furati.
Wakimbizi hao walikimbia makazi yao kufuatia mapigano makali ya hivi karibuni baina ya kikundi cha kigaidi cha Daesh na majeshi ya Syria katika mji wa Deir ez-Zor, ambapo lengo la majeshi ya Syria ni kuikomboa sehemu hiyo kutoka mikononi mwa kikundi cha Daesh.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky